Alhamisi, 3 Julai 2014

MAHALI SAHIHI PA KUTOLEA SADAKA

MASWALI NA MAJIBU NDANI YA BIBLIA

BWANA YESU ASIFIWE SANA!!

Ningependa kujibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wasomaji wa blogspot hii,kupitia barua pepe (gervasshayo@gmail.com), kuhusu BIBLIA..

Naamini kabisa majibu haya yatakupa mwanga na njia sahihi ya kupata ufafanuzi.

SWALI LA KWANZA:
"..
Kwa mfano, siku ya ibada NIKATOA SADAKA KWA MJANE AU YATIMA badala ya kotoa kanisani.Je, nitakuwa sahihi?
MAJIBU

Kwa mujibu wa swali hili utaelewa kuwa huyu ndugu anahitaji kujua MAHALI SAHIHI PA KUTOA SADAKA.

Biblia inasema katika Yakobo 1:27...."Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao......" Hapa biblia haijasema kuwapa sadaka yatima na wajane bali kuwasaidia katika dhiki zao. Unapomsaidia yatima au mjane, haujampa sadaka bali umemsaidia kama biblia inavyosema.

SADAKA ni matoleo yanayotolewa na mwanadamu kwa kumrudishia mungu shukrani.

AINA ZA SADAKA

  1. Sadaka ya kawaida: Hii ni sadaka ambayo mwanadamu anatoa kwa Mungu kushukuru kwaajili ya kumuongoza na kumlinda kwa wiki nzima.
  2. Sadaka ya FUNGU LA KUMI na ZAKA: Hizi ni sadaka ambazo ni lazima kutoa tena kwa ukamilifu. Malaki 3:7-10..."   Pia soma    Matendo 5:1-10 ...utaona habari za ANANIA na SAFIRA mkewe ambao wote walikufa mbele ya mitume (petro) kwa kosa la kutokutoa walicho ahidi kwa ukamilifu na kujaribu kuficha sahemu ahadi yao kwa siri..
  3. Nadhiri na ahadi: kumbukumbu 23:21-23."...Utakapoweka nadhiri kwa Bwana, Mungu wako, Usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa Bwana, Mungu wako,hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.......23,...yaliyotoka mdomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano uliyomwekea nadhiri Bwana,Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako....."
  4. Malimbuko: Hii ni sadaka ya mzaliwa wa kwanza. (a) Mshahara wako wa kwanza (kama mzaliwa wa kwanza) wote- sadaka kwa Mungu   (b)  Faida ya mapato ya kwanza-biashara, kilimo..  Mithali 3:9-10 .. ."...mheshimu Bwana kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote. ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi....Pia soma Nehemia 12:44 , kumbukumbu 26:1-2  ,  2nyakati 31:4-6
  5. Dhabihu : Hii ni sadaka ambayo roho mtakatifu husema na wewe moja kwa moja.. mwanzo 22:1-3... utaona habari za Ibrahimu


Tunapaswa kutoa sadaka wapi?

Mahali sahihi pa kutoa sadaka ni KANISANI yaani nyumba ya Mungu...
Kumbukumbu 12:5-7...."...Lakini mahali atapochagua BWANA, Mungu wenu, ...maana ni makao yake,elekezeni nyuso zenu huko,nawe wende huko;pelekeni huko sadaka zenu...na dhabihu zenu , na zaka zenu....nadhiri zenu na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza...."

Kwanini tunatoa sadaka?

a) Kutoa sadaka ni agizo la Mungu- kumbukumbu 8:6
Kutoka 25:1-2.."..Mungu akanena na Musa, waambie wana wa israeli kwamba wanitwalie sadaka......:

b) Kutoa sadaka ni kuonyesha utii kwa Mungu..
Unapotii unapata...kumbukumbu 28:1-8.... na usipo tii unapata haya... kumbukumbu 28:15-22.
Pia soma Matendo 4:34-36...utaona jinsi watu wakitoa kwa uaminifu
Matendo 5:1-10...utapata habari za anania na safira..

Kwahiyo, kutoa sadaka ni muhimu na pia kusaidia wajane na yatima ni muhimu..Unapomsaidia mtu mwenye shida haimaanishi kwamba umetoa sadaka bali umemsaidia kwahiyo kutoa sadaka kuko palepale... ukisoma MALAKI 3:7-10... Mungu anamfananisha mtu asiyetoa sadaka na mwizi... tena anasema.."...mne niibia zaka na dhabihu,ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi...."

NAAMINI KABISA, UMEPATA MAJIBU MAZURI KABISA....

Imeandaliwa na:
Gervas Shayo 
0756415776
gervasshayo@gmail.com. (tuma swali lako kupitia hii barua pepe na litakuwa msaada kwa wengi)

MUNGU AKUBARIKI SANA!!

ENDELEA KUSOMA MACHAPISHO YAJAYO NITAKUWA NAENDELEA KUJIBU BAADHI YA MASWALI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni