Alhamisi, 3 Julai 2014

MAHALI SAHIHI PA KUTOLEA SADAKA

MASWALI NA MAJIBU NDANI YA BIBLIA

BWANA YESU ASIFIWE SANA!!

Ningependa kujibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wasomaji wa blogspot hii,kupitia barua pepe (gervasshayo@gmail.com), kuhusu BIBLIA..

Naamini kabisa majibu haya yatakupa mwanga na njia sahihi ya kupata ufafanuzi.

SWALI LA KWANZA:
"..
Kwa mfano, siku ya ibada NIKATOA SADAKA KWA MJANE AU YATIMA badala ya kotoa kanisani.Je, nitakuwa sahihi?
MAJIBU

Kwa mujibu wa swali hili utaelewa kuwa huyu ndugu anahitaji kujua MAHALI SAHIHI PA KUTOA SADAKA.

Biblia inasema katika Yakobo 1:27...."Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao......" Hapa biblia haijasema kuwapa sadaka yatima na wajane bali kuwasaidia katika dhiki zao. Unapomsaidia yatima au mjane, haujampa sadaka bali umemsaidia kama biblia inavyosema.

SADAKA ni matoleo yanayotolewa na mwanadamu kwa kumrudishia mungu shukrani.

AINA ZA SADAKA

  1. Sadaka ya kawaida: Hii ni sadaka ambayo mwanadamu anatoa kwa Mungu kushukuru kwaajili ya kumuongoza na kumlinda kwa wiki nzima.
  2. Sadaka ya FUNGU LA KUMI na ZAKA: Hizi ni sadaka ambazo ni lazima kutoa tena kwa ukamilifu. Malaki 3:7-10..."   Pia soma    Matendo 5:1-10 ...utaona habari za ANANIA na SAFIRA mkewe ambao wote walikufa mbele ya mitume (petro) kwa kosa la kutokutoa walicho ahidi kwa ukamilifu na kujaribu kuficha sahemu ahadi yao kwa siri..
  3. Nadhiri na ahadi: kumbukumbu 23:21-23."...Utakapoweka nadhiri kwa Bwana, Mungu wako, Usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa Bwana, Mungu wako,hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.......23,...yaliyotoka mdomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano uliyomwekea nadhiri Bwana,Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako....."
  4. Malimbuko: Hii ni sadaka ya mzaliwa wa kwanza. (a) Mshahara wako wa kwanza (kama mzaliwa wa kwanza) wote- sadaka kwa Mungu   (b)  Faida ya mapato ya kwanza-biashara, kilimo..  Mithali 3:9-10 .. ."...mheshimu Bwana kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote. ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi....Pia soma Nehemia 12:44 , kumbukumbu 26:1-2  ,  2nyakati 31:4-6
  5. Dhabihu : Hii ni sadaka ambayo roho mtakatifu husema na wewe moja kwa moja.. mwanzo 22:1-3... utaona habari za Ibrahimu


Tunapaswa kutoa sadaka wapi?

Mahali sahihi pa kutoa sadaka ni KANISANI yaani nyumba ya Mungu...
Kumbukumbu 12:5-7...."...Lakini mahali atapochagua BWANA, Mungu wenu, ...maana ni makao yake,elekezeni nyuso zenu huko,nawe wende huko;pelekeni huko sadaka zenu...na dhabihu zenu , na zaka zenu....nadhiri zenu na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza...."

Kwanini tunatoa sadaka?

a) Kutoa sadaka ni agizo la Mungu- kumbukumbu 8:6
Kutoka 25:1-2.."..Mungu akanena na Musa, waambie wana wa israeli kwamba wanitwalie sadaka......:

b) Kutoa sadaka ni kuonyesha utii kwa Mungu..
Unapotii unapata...kumbukumbu 28:1-8.... na usipo tii unapata haya... kumbukumbu 28:15-22.
Pia soma Matendo 4:34-36...utaona jinsi watu wakitoa kwa uaminifu
Matendo 5:1-10...utapata habari za anania na safira..

Kwahiyo, kutoa sadaka ni muhimu na pia kusaidia wajane na yatima ni muhimu..Unapomsaidia mtu mwenye shida haimaanishi kwamba umetoa sadaka bali umemsaidia kwahiyo kutoa sadaka kuko palepale... ukisoma MALAKI 3:7-10... Mungu anamfananisha mtu asiyetoa sadaka na mwizi... tena anasema.."...mne niibia zaka na dhabihu,ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi...."

NAAMINI KABISA, UMEPATA MAJIBU MAZURI KABISA....

Imeandaliwa na:
Gervas Shayo 
0756415776
gervasshayo@gmail.com. (tuma swali lako kupitia hii barua pepe na litakuwa msaada kwa wengi)

MUNGU AKUBARIKI SANA!!

ENDELEA KUSOMA MACHAPISHO YAJAYO NITAKUWA NAENDELEA KUJIBU BAADHI YA MASWALI

Jumapili, 1 Juni 2014

TAMBUA NGUVU ILIYOPO KATIKA KINYWA CHAKO

Bwana Yesu asifiwe Wana wa Mungu.
Napenda kuleta kwenu somo hili:

TAMBUA NGUVU YA MUNGU ILIYOPO KATIKA KINYWA CHAKO. 

Je Unakirinini?

“Nanyi mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu,(Matendo1:8).Je, tunatumia hii nguvu ya Mungu na mamlaka tuyopewa kama inavyotakiwa?”

Haijalishi mwana wa Mungu unapita katika magumu kiasigani, unachotakiwa ni kubadilisha kukiri kwako,  na kadri unavyotamka kinyume na mazingira yanavyoonekana, elewa kunajambo katika ulimwengu wa Roho linafanyika, hatakama hunashilingimia mfukoni wewe sema pesa zipo, hatakama wewe ni mgonjwa umelala kitandani Sema mimi ni mzima, maana. Neno la Mungu linasema “aliyedhaifu na aseme ana nguvu”.

Ezekieli alipoonyeshwa lilebonde la mifupa mikavu, kwa macho ya damu na nyama aliona haiwezekani kwa ile mifupa mikavu kuwa na uhai tena , lakini Mungu akamwambia itabirie hii mifupa mikavu ipate kuishi. Ndipo Ezekieli akatambua nguvu iliyopo katika kinywa chake, akaanza kutoa unabii nakuitabiria ile mifupa, akaiambia “…enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la BWANA; Bwana MUNGU aniambia mifupa hii maneno haya; Tazama nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi .Nami nitatia mishipa juu yenu, nam initaleta nyama iwe juu yenu, nakuwafunika ngozi, nakutia pumzi ndani yenu nanyi mtaishi…” Maneno haya tunayapata katika kitabu cha (Ezekieli 37:1…..)
Katika maandiko haya tumeona, ni  jinsi gani Ezekieli alivyoweza kutumia nguvu nauweza ulioko ndani ya kinywa chake na kuweza kuleta uhai tena.

Na wewe mwana wa Mungu ninini kimekuwa mifupa mikavu katika maisha yako?
Yumkini ni ndoa ndio imekuwa mifupa mikavu itabirie nayo itakuwa hai tena, au ni
- Uchumi wako,
- Afya yako,
- Watoto wako,
-Huduma yako, Mungu ana kuambia leo simama na uvitabirie,  maana kunanguvu katika kutamka.
Usikubali kukiri kushindwa ,Nguvu ya Mungu iko juu yako, badilisha yale yote yanayo onekana kuwa yameshindikana na yatawezekana kupitia kinywa chako katika Jina la YESU KRISTO.  AMEEEN.

Mungu akubariki sana.

Emma E. Lyimo.
Cell: 0756 496 496


Jumatano, 21 Mei 2014

HE KNOWS MY NAME Lyrics

HE KNOWS MY NAME

I have a maker
He formed my heart
Before even time begin
My life was in his hand

                                                
                                                      (Chorus)

He knows my name
He knows my every thought
He sees each tear that falls
And hears me when i call


I have a father
He calls me his own
He'ii never leave me
No matter where I go.

( chorus )x.....

Alhamisi, 15 Mei 2014

MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU

Namshukuru Mungu muweza wa yote kwajili ya uzima tulio nao.Hakika ukisoma blog spot hii,hutabaki ulivyo maana Mungu atabadilisha maisha yako kupitia MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU hapa.Pia kutakuwa na masomo na ushauri kwajili ya watu wanao hitaji kumtumikia MUNGU kwa njai ya UIMBAJI..hakika uimbaji wako utabadilika na utakuwa wa baraka sana.Usikose makala zijazo,Mungu akupe neema na kibali..

Kwenye blog spot hii,utaanza kupata huduma zifuatazo
1:MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU(MARKO 16:15-16)
2:MASOMO NA USHAURI UIMBAJI
3:MAOMBEZI KWA WATU WENYE SHIDA MBALIMBALI..

AMANI YA KRISTO IWE NAWE...!

ISAYA 26:4
YEREMIA 33:3

Alhamisi, 6 Februari 2014

THE POWER OF FORGIVENESS

~Don't forget to forgive.
"When your praying,first forgive anyone you are holding a grudge agaist,so that your father in heaven will forgive your sins too.(MARK 11:25)
~What does forgiveness looks like?
*some describe it as giving up the right to revenge or the obligation to "get even".Parhaps you have heared the phrase "forgive and forget".
~I think Gods forgiveness looks more than that,because he said himself "I will blot out your sins and i will never think of them again"(ISIAH 43:25)

Prepared by
Gervas shayo
gervasshayo@gmail.com

NIMEKUWA MACHO by GERVAS SHAYO

Jipatie cd ya albamu yangu ya pili,inayoitwa NIMEKUWA MACHO ambayo kwa sasa ipo madukani.Albamu hii ina nyimbo takribani nane(8)
1:NITAKASE
2:IKO WAPI AMANI
3:NIMEITWA NA YESU
4:NITEMBEE NA YESU
5:NIMEKUWA MACHO
6:MOYO SAFI
7:ANAWEZA
8:DUNIA INAPITA
Kwa maelezo zaidi wasiliana nami GERVAS SHAYO
+255756415776 au +255654310133,
pia email:gervasshayo@gmail.com
                 gervasfesto@yahoo.com
MUNGU AKUBARIKI SANA....
  Mwaka 2014 uwe mwaka wa MAVUNO kwako..

NIMEKUWA MACHO