Jumapili, 1 Juni 2014

TAMBUA NGUVU ILIYOPO KATIKA KINYWA CHAKO

Bwana Yesu asifiwe Wana wa Mungu.
Napenda kuleta kwenu somo hili:

TAMBUA NGUVU YA MUNGU ILIYOPO KATIKA KINYWA CHAKO. 

Je Unakirinini?

“Nanyi mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu,(Matendo1:8).Je, tunatumia hii nguvu ya Mungu na mamlaka tuyopewa kama inavyotakiwa?”

Haijalishi mwana wa Mungu unapita katika magumu kiasigani, unachotakiwa ni kubadilisha kukiri kwako,  na kadri unavyotamka kinyume na mazingira yanavyoonekana, elewa kunajambo katika ulimwengu wa Roho linafanyika, hatakama hunashilingimia mfukoni wewe sema pesa zipo, hatakama wewe ni mgonjwa umelala kitandani Sema mimi ni mzima, maana. Neno la Mungu linasema “aliyedhaifu na aseme ana nguvu”.

Ezekieli alipoonyeshwa lilebonde la mifupa mikavu, kwa macho ya damu na nyama aliona haiwezekani kwa ile mifupa mikavu kuwa na uhai tena , lakini Mungu akamwambia itabirie hii mifupa mikavu ipate kuishi. Ndipo Ezekieli akatambua nguvu iliyopo katika kinywa chake, akaanza kutoa unabii nakuitabiria ile mifupa, akaiambia “…enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la BWANA; Bwana MUNGU aniambia mifupa hii maneno haya; Tazama nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi .Nami nitatia mishipa juu yenu, nam initaleta nyama iwe juu yenu, nakuwafunika ngozi, nakutia pumzi ndani yenu nanyi mtaishi…” Maneno haya tunayapata katika kitabu cha (Ezekieli 37:1…..)
Katika maandiko haya tumeona, ni  jinsi gani Ezekieli alivyoweza kutumia nguvu nauweza ulioko ndani ya kinywa chake na kuweza kuleta uhai tena.

Na wewe mwana wa Mungu ninini kimekuwa mifupa mikavu katika maisha yako?
Yumkini ni ndoa ndio imekuwa mifupa mikavu itabirie nayo itakuwa hai tena, au ni
- Uchumi wako,
- Afya yako,
- Watoto wako,
-Huduma yako, Mungu ana kuambia leo simama na uvitabirie,  maana kunanguvu katika kutamka.
Usikubali kukiri kushindwa ,Nguvu ya Mungu iko juu yako, badilisha yale yote yanayo onekana kuwa yameshindikana na yatawezekana kupitia kinywa chako katika Jina la YESU KRISTO.  AMEEEN.

Mungu akubariki sana.

Emma E. Lyimo.
Cell: 0756 496 496